‘Sikujua Ni Kwa Namna Gani Nilipata Mimba’ Swahili Summary Report

Mimba na ndoa za utotoni ni mojawapo ya changamoto kubwa za kiuchumi na kijamii zinazoikabili Wilaya ya Mpwapwa, iliyo Mkoa wa Dodoma, Tanzania. Kuwapa mimba wasichana katika umri mdogo kabla ya ndoa, na wakati mwingine kuwalazimisha kuolewa bila ridhaa yao inasababisha kuwepo kwa majanga ya kiuchumi na kijamii nchini. Tatizo hili linazuia fursa na ndoto za wasichana sanjari na kusababisha umasikini endelevu na kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia.