Simulizi ya Kweli ya Ghati na Rhobi ni filamu ya uhuishaji ya dakika tano inayolenga kuongeza uelewa juu ya ukeketaji. Inaeleza simulizi ya kuvutia ya wasichana wawili (Ghati na Rhobi) ambao walikaataa ukeketaji kwenye jamii yao. Wasichana hawa walionyesha ujasiri kwa kusema hapana kwa ukeketaji, kitendo ambacho walisikia kina maumivu makali ambapo wasichana kadhaa hufariki kutokana nacho. Kwa msaada wa wazee katika jamii yao, walibadilisha mitazamo juu ya kipindi cha mpito cha msichana kutoka usichana kwenda utu uzima yaani kuwa mwanamke kwa kutokomeza ukeketaji.
Toleo la kiingereza: The True Story of Ghati and Rhobi
Imetengenezwa na FORWARD na Animage Films kwa kushirikiana na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto Forum (CDF). Imefadhiliwa na Comic Relief na Sigrid Rausing Trust. Imetengenezwa na kuongozwa kwa ushirikiano wa the award winning filmmaker na mwansidhi Ruth Beni. Imehuishwa na Yael Ozsinay. Santuri na Muziki kutoka kwa msanii wa Kongo Mulele Matondo Afrika: www.mulelematondo.com
Changia kusaidia FORWARD kutokomeza ukeketaji! Tafadhali andika FWRD30 £ 3 (au kiasi kingine) kwenda na : 70070
Iwapo utahitaji msaada kuhusu masuala yaliyowakilishwa katika filamu hii, tafadhali wasiliana na FORWARD kwa namba 020 8960 4000 (Mkondo 1), au [email protected]. Nchini Tanzania tafadhali wasiliana na CDF: Simu namba: +255 (0) 22 2 775 010.
Filamu hii inaweza kutumika kwa minajili ya kitaaluma na kuelimisha, tafadhali andika barua pepe kwa [email protected] kupata toleo linaloweza kupakuliwa na maelezo jinsi ya kutumia filamu hii. Iwapo upo Tanzania tafadhali andika barua pepe: [email protected] iwapo utahitaji DVD na mwongozo wa mwezeshaji na utoe maelezo jinsi utakavyotumia filamu hii.
Kwa maelezo zaidi: http://www.forwarduk.org.uk http://www.cdftz.org http://www.animageltd.com